HabariPilipili FmPilipili FM News

Tahadhari Ya Mvua Kubwa Yatolewa Pwani

Kaunti za mombasa, Kwale, kilifi , Lamu na Taita-Taveta ni miongoni mwa kaunti ambazo zinatarajiwa kushuhudia mvua kubwa kuanzia hii leo hadi mwishoni mwa juma hili.

Ripoti ya hivi karibuni ya  idara ya utabiri wa hali ya hewa pia imeyataja maeneo ya Nairobi, magharibi mwa nchi, Nyanza na sehemu za bonde la ufa, kuwa miongoni mwa sehemu zitakazoshuhudia mvua kubwa.

Maeneo mengine yaliyotajwa ni kaskazini na kusini mashariki mwa nchi, pamoja na maeneo ya pwani na kati, ambayo tayari yanaendelea kushuhudia mvua.

Ripoti hiyo imeashiria kuwa huenda maeneo kadha yakashuhudia mafuriko, huku kiwango cha mvua kikitarajiwa kufikia milimita 40 kwa saa 24.

Show More

Related Articles