BiasharaPilipili FmPilipili FM News

Shirika La Majani Chai Mombasa Lapata Ushindani.

Shirika la kusambaza majani chai Afrika mashariki kutoka kaunti ya Mombasa linakabiliana na ushindani mkubwa miongoni mwa nchi nyengine  za Afrika mashariki ikizingatiwa shirika hilo ndilo lenye majani chai bora Afrika nzima.

Mahitaji ya majani chai yameonekana kupanda kwa asilimia 4 lakini imeathiri bei ya kusafirisha bidhaa hio katika bara la Afrika na hata ulimwengu mzima.

Aidha shirika hilo linapania kuuza bidhaa zake katika nchi nyengine kwa kutumia pakiti ili kuongeza thamani ya bidhaa hio ya majani chai kwani kuuza kwa magunia thamani ya bidhaa hio inashuka.

Vinara kutoka mashirika mbalimbali wamesema kuwa iwapo  kutakuwa na maadili ya uhalali na uwazi katika biashara hio huwenda mahitaji ya bidhaa hio ikaongezeka zaidi.

Show More

Related Articles