BurudaniPilipili FmPilipili FM News

RAY C Aomba Serikali Ya Kenya Kuekeza Zaidi Katika Vituo vya Kuwatibu Waathiriwa Wa Mihadharati.

Mwanamziki Wa kizazi kipywa kutoka nchini Tanzania Rehema Chalamila almaarufu RAY C ameitaka serikali ya Kenya kujenga vituo vingi vya kuwatibu waathiriwa Wa mihadarati pamoja na kuwekeza katika kampeni ya kuhamasisha umma juu ya athari za dawa za kulevya

Akiongea hapa mjini Mombasa kwenye sherehe za kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupambana na utumizi na ulanguzi Wa dawa za kulevya,Ray C ambaye pia ni mhanga wa uraibu wa mihadarati, amewataka wazazi kukoma kuwaficha watoto wao walioathirika badala yake kuwataftia matibabu

Kauli hii ineungwa mkono na Raisi wa Vijana kaunti ya mombasa Alfred Otieno pamoja na mkrugenzi katika Shirika LA NACADA Vincent Mwasia Almaarufu  Chipukizi ambao wote wamesema ni lazima jamii na serikali isimame pamoja kuwakomboa vijana.

 

Show More

Related Articles