HabariPilipili FmPilipili FM News

Raila Amezindua Mpango Wa Huduma Namba Mombasa.

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amezindua rasmi usajili wa huduma namba kaunti ya Mombasa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Raila amewahimiza wakaazi wote kujitokeza kijiandikisha ili kuwawezesha kupata huduma za serikali kirahisi.

Wakti huo huo Raila amekinzana na kauli ya majaji waliotoa uamuzi wao jana ambapo kwenye uamuzi huo waliitaka serikali isiwashurutishe wananchi kwenye zoezi hili akisema zoezi hili ni mhimu kwa kila mwananchi hivyo wananchi wote wanatakiwa kupata huduma namba.

Uzinduzi huu unajiri huku pia rais Uhuru Kenyatta akiwa kaunti ya Machakos naye naibu wake William Ruto akiwa kaunti ya Kakamega kwa hafla kama hiyo nao viongozi wa Wiper na ANC Kalonzo Msyoka na Msalia mudavadi wakiwa Murang’a na Kajiado mtawalia.

Zoezi hili limeanza leo na linatarajiwa kukamilika tarehe 17 mwezi ujao.

Show More

Related Articles