MakalaPilipili FmPilipili FM News

Wauzaji Mugukaa Walalamikia Kutozwa Ada Za Juu, Mombasa.

Hisia mseto zinaendelea kuibuka miongoni mwa wauzaji wa Mogokaa kaunti ya mombasa wengi wao wakidai kukabiliwa na changamoto nyingi hasa baada ya serikali ya kaunti kuongeza kodi inayotozwa bidhaa hiyo.

Wengi wamelalamikia ada za juu wanazotozwa na maafisa wa kaunti pamoja na mazingira mabaya ya soko, na katika baadhi ya sehemu wauzaji wakinyimwa sehemu za kufanyia biashara zao.

Itakumbukwa kuwa serikali ya kaunti ya mombasa iliongeza kodi inayotozwa Mogokaa ndani ya kaunti ya mombasa, ili kujaribu kuthibiti watumizi wa bidhaa hiyo kwa madai kuwa ina athari za kiafya, japo hilo bado halijathibitishwa.

Show More

Related Articles