HabariPilipili FmPilipili FM News

Rais Uhuru Kenyatta Apiga Kura Yake

Rais  Uhuru Kenyatta  amepiga kura yake eneo la gatundu kaunti ya kiambu.

Akiongea mda mfupi tu baada ya kupiga kura yake rais amewataka wananchi kupiga kura kwa amani bila wasiwasi akisema hiyo ni haki ya kila mkenya kikatiba.

Rais Kenyatta amesema demokrasia katika taifa la Kenya imekua kwa kiasi kikubwa akiongeza kuwa maamuzi ya wakenya yanafaa kuheshimiwa kwani kila mtu ana haki ya kupiga ama kutopiga kura.

Rais Kenyatta aidha ametaka maafisa wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC waruhusiwe kutekeleza wajibu wao kama tume huru bila kuingililiwa kwa njia yoyote ile.

Show More

Related Articles