HabariPilipili FmPilipili FM News

Bodi Ya Kuzuia Biashara Haramu Katika Kaunti Ya Taita Taveta Ya Buniwa

Kaunti ya Taita Taveta inanuia kubuni bodi maalum itakayotwikwa jukumu la kutathmini uhalali wa mali inayomilikiwa kwenye ranch zote kaunti hiyo.

Kulingana na Gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja itaweka wazi shughuli zinazoendeshwa katika renchi zote hivyo kuzuia biashara haramu ikiwemo kuingiza ng’ombe kutoka nje kimagendo swala linalochangia kuongezeka mizozo katika ya jamii na wanyamapori.

Samboja amesema licha ya kaunti hiyo kuwa huru kutokana na magonjwa ya mifugo, maafisa wa idara ya ukulima na ufugaji wameelezea wasiwasi wa mikurupuko ya magonjwa ya mifugo kwani  idadi kubwa ya ngamia na ng’ombe wanaoingizwa kutoka kaunti za nje hawana chanjo.

Show More

Related Articles