Serikali Ya Kaunti Ya Kilifi Ya Pewa Makataa Ya Siku Tatu

Serikali Ya Kaunti Ya Kilifi Ya Pewa Makataa Ya Siku Tatu
PilipiliPhotography

Zaidi ya wakazi elfu 30 katika wadi ya Sabaki kaunti ya kilifi wameipa serikali ya kaunti hiyo makataa ya siku tatu, kusitisha mradi unaoendeshwa katika mojawapo ya shamba la kilimo cha umma huko kisiwani, la sivyo watalazimika kuitisha maandamano kupinga mradi huo.

Wakazi hao wanadai zaidi ya ekari 900 za ardhi ya umma zimenyakuliwa na mabwenyenye eneo hilo.

Also read:   Mutongoria wa bururi Uhuru Kenyatta gutwara kambe-ini cia Jubilee gicua-ini

Wakiongozwa na mwakilishi wadi wa eneo hilo Edward Kazungu wanasema tayari wamewaandikia gavana Amason Kingi pamoja na mbunge wa ene hilo Michael Kingi, mshirikishi wa serikali pwani miongoni mwa wengine kuhusu suala hilo.

Kazungu amemlaumu machifu pamoja na mkurugenzi wa idara ya maji mjini malindi Gerald Mwambire , kwa kupanga kunyakua ardhi hiyo kwa ajili ya mabwenyenye

Also read:   Wakandarasi Waonywa Kilifi.

Post source : Pilipilifm

Related posts

MNL App
MNL App