HabariPilipili FmPilipili FM News

Mawaziri Walioteuliwa Wazidi Kupigwa Msasa

Shughuli ya kuwapiga msasa mawaziri walioteuliwa na rais Uhuru Kenyatta imeingia siku ya pili hii leo, ambapo kwa sasa Kerikao Tobiko amefika mbele ya kamati iliyoteuliwa.

Tobiko ambaye alikuwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma ameteuliwa kushikilia wizara ya mazingira.

Akijieleza Tobiko amesema ana kipaji cha kushikilia wizara hiyo akisema inahitaji mtu kama yeye.

Also read:   Walioteuliwa Kuhudumu Kama Mawaziri Kupigwa Msasa Hapo Kesho

Wengine wanaotarajiwa kupigwa msasa huo hii leo ni pamoja na Rashid Achesa ambaye aliteuliwa kusimamia wizara ya michezo, Ukur Yattany katika wizara ya leba pamoja na waziri Simon Chergui katika wizara ya maji na unyunyuziaji

Kikao hicho cha kuwakagua mawaziri hao wateule kinachoongozwa na spika wa bunge Justin Muturi kinakamilisha zoezi hilo leo.

Also read:   Rais Uhuru Kenyatta awaonya makatibu wapya wa wizara
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker