BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Nipo Kibiashara Sipo Kwa Ubishoo, Asema TK2.

Nimekuja kivyengine na nia yangu nikuhakikisha production ya mziki wa pwani inakua tofauti kabisa, haya ni maneno ya producer mkali kutoka Mombasa TK2.

Mzalishaji huyo wa nyimbo ambaye pia ni mwanamziki ameapa kuhakikisha anawacha alama yenye kuigwa kwenye mziki wa Coast.

Kusema kweli mziki umebadilika sana na nia yangu nikwenda na wakati ndio mana ukicheck mziki ninaotoa kwa wasanii wanaopitia kwangu unaladha tofauti na hilo ndilo nalifanya kwa sasa. Amesema TK2

Kwa sasa yeye na City Boy wanatamba na nyimbo yao mpya “Wanajileta” nyimbo ambayo imekuja na mtindo tofauti ikilinganishwa na zile amezitoa awali.

Kuhusu kufanya kazi na aliyekua msanii wa kundi lilovunjika la Yamoto Band  Enock Bella, TK2 amekiri nikweli msanii huyo amependezwa na midunzo na kazi zake na ameamua kutoa baadhi ya nyimbo ndani ya studio za Number One.

TK2 aidha amepinga madai ya baadhi ya wasanii wanaodai yeye ni producer mkali ila kasoro yake analaza sana kazi.

Akiongea na meza ya soga producer huyo amepinga madai hayo akisema yeye anafanya kazi na wasanii ambao pia wako tayari kujitolea kufanya mziki kama kazi wala si ubisho huku akitoa mfano wa Bawazir kuwa ni msanii ambaye yupo kibiashara so anafaa aeleweke kwa hilo.

Producer huyu atakumbukwa kwa kuwahi mzalishia nyimbo MB Doggy Man kutoka Tanzania na pia nyimbo za Ngoma itambae na Hidaya za Susumila akimshirikisha Chikuzee na sasa ameahidi makubwa mwisho wa mwaka huu na mwaka ujao wote.

Show More

Related Articles