BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Ninamvuto Na Nyota Yakupendwa Na Wanawake,Asema Msanii Brown Mauzo.

Baada yakupotea kwa muda mrefu  huku ikidaiwa alikua na uhusiano wa kimapenzi na mkw wa meneja wake, msanii Brown Mauzo amekiri kuwa muonekano na mvuto wake ndio sababu kuu ya yeye kupendwa na wanawake tofauti tofauti.

Akihojiwa kwenye kipindi cha Mishemishe ndani ya Pilipili fm msanii huyo amekiri bayana kuwa ananyota ya kupendwa.

Mimi sijilaumu ila ninamvuto na  nyota yakupendwa na wanawake na kati ya wasanii wote hapa Kenya mimi ndo namvuto so hata watu walalamike haitosaidia”, Amesema Mauzo.

Na amekiri hewani anampenda sana Wema Sepetu na kutokana na mvuto na nyota aliyonayo, Wema atakubali maombi yake.

Kuhusiana na msanii Kelechi Africana,Mauzo ameweka bayana kutomtambua msanii huyo na taarifa zilizozagaa kumhusu yeye na Kelechi kuwa anajifanya ni uongo kwa sababu yeye hamjui kiukweli na hajui nyimbo zake.

Lakini mzozo huo ulitatuliwa baada ya Kelechi kuwekwa live hewani nakuongea na Mauzo na kuweka mambo wazi ambapo wameahidiana kufanya kazi pamoja.

Aidha msanii Mauzo amemhimiza Kelechi kuingia gym nakutengeneza muonekano na afanye mziki mzuri kwa mashabiki.

Wakati huohuo msanii huyo amedokeza kuwa kila mwezi atakua akiachilia nyimbo ili kurudisha imani yake kwa mashabiki wake ambao amewataja kuwa na kiu ya mziki wake.

Show More

Related Articles