BurudaniPilipili FmPilipili FM News

“Mwanamke Hajanifanya Nitoke Kubwa Entertainment”, Kelechi Africana.

Mwaka wa 2018 umekua mwaka wa mafanikio makubwa kwa msanii Kelechi baada yakujitafuta kwa kipindi kirefu alianza kukubalika mwaka Jana.

Akiwa chini ya usimamizi wa kubwa studio Kelechi alishamiri na kuwa mmoja wa wasanii tajika 2018 lakini sasa ni rasmi amejitoa kwenye kubwa studio nakuanza himaya yake anayoiita fleekboss.

Kujitoa kwa msanii huyo ndani ya kubwa kumeonekana kuzua mjadala huku Athman Babaz mmiliki wa kubwa akizungumza na meza ya soga amesema wazi kuwa Kelechi hajamjulisha kuhusu hilo na aliona kwa mitandao ya kijamii tu.

“Mimi kusema kweli kaka sijaongea na Kelechi na kuhusu kujitoa nimeona kwa mitandao na kusema kweli msanii huyu nimehangaika na yeye nikiwa na hali ngumu ya kifedha mpaka ameanza kujielewa but sai ameonelea sistahili kuvuna matunda ” Amesema Babaz.

Kelechi African itakumbukwa nyimbo iliyomtambulisha kwa mara ya kwanza ni nyimbo ya Nitalia aliyoshirikishwa na wasojali wakati huo na kisha baadae kundi lilisambaratika  na Babaz akamuchukua kelechi nakuanza utawala mpya ndani ya Kubwa Studios.

Kwa kipindi chote msanii huyo ameonyesha kunyenyekea lakini mwishoni mwa mwaka jana kulingana na Babaz alianza kuonyesha utofauti na tabia ya kumdharau meneja wake.

Mapema mwaka huu hili lilizidi kiasi cha kulenga simu za Babaz bila sababu.

Kelechi amekua akilenga simu zangu mara anawapatia vijana wake waongee na mimi amenibadilikia sana ameongeza Babaz.

Lakini mdakuzi wetu anaeleza kuwa chanzo cha Kelechi kuvimba makwapa ni kwa sababu kuna mwanadada mwenyewe fulusi na inaaminika ameanza kumsimamia na sai ashamfungulia studio ya mziki jijini Nairobi na inadaiwa huenda penzi la mwanadada huyo anayeishi Italia ndio chanzo cha kuamua kuachana na wasimamizi wake wa zamani.

Ikumbukwe Kelechi aliachana na mama mtoto wake hapo awali, na hivi majuzi alishindwa kuficha hisia zake kwa mpenzi wake wa sasa na akaamua kuanika kila kitu kwa kuandika ujumbe mzito wa mapenzi kwenye matandao wa Instagram.

Kwa upande wake msanii huyo amejitetea akisema hajatoka kwa ubaya ila ukosefu wa juhudi za kusukuma kazi zake ndio chanzo na wala hajutii kufanya kazi ya Babaz.

Kuhusu mwanadada kumvimbisha kichwa Kelechi amekanusha hilo akisema alikua na nia ya kutoka Kubwa studios kitambo na alingoja wakati mwafaka.

“Mimi mwanamke anayesema amenifanya nitoke kwake sijamuona na kitu nitasema niko na mpenzi wangu ambaye nampenda sana na mbona angoje nitoke ndio  asema hivyo mimi nimeamua kusimama kivyangu na niko na studio yangu sasa”. Amenean Kelechi.

Aidha Kelechi amekanusha madai yakumuonyesha dharau Babaz akisema hajawahi kumdharau wala hawezi kwa sababu amemsaidia na anamchukulia kama kakake mkubwa.

 

 

Show More

Related Articles