BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Musa Babaz Amenitelekeza Kimziki Asema Msanii D-Rush.

Kwa wengi husema ukiwa na mtu katika tasnia yoyote ambaye anauwezo wakukusaidi basi hufai kujituma zaidi lakini hio ni tofauti kwa msanii D-Rush kutoka Mombasa.

Msanii huyu ambaye kakake mkubwa ni promoter mkubwa Afrika mashariki Musa Babaz amedokeza kuwa bado hajapata msaada wowote kutoka kwa kakake huyo akisema amemtelekeza.

Akihojiwa ndani ya kipindi cha mwake mwake msanii huyo amemwaga razi kwa kusema kuwa ndugu wa Musa Babaz haimanishi atulie angoje nyimbo zake zisukumwe na Babaz.

Mimi Musa ni ndugu yangu kabisa tumbo moja na kuna vitu siezi sema lakini kiukweli hajanisaidia hata kidogo hata kuna wakati nilitoa ngoma yangi kali na video lakini akaiua haikutoka kabisa so mimi nasukuma mziki kivyangu bila kumtegemea yeye. Amsema D-Rush.

Kuhusu kama anakifua cha kupigana na changamoto za mziki nchini amesema yeye amejitolea mhanga kuhakikisha kuwa mziki wake hausikikitu kanda ya pwani bali Kenya nzima kwa ujumla huku akiwaahidi mashabiki wake kua huu ni mwanzo mazuri zaidi yanakuja.

Kwa sasa msanii huyo anatamba na kibao kipya kwa jina Sinyorita ambacho kimezalishw na producer mkali Amz wa leo ndani ya studio za Namaan music.

Namaan music studio ni moja ya studio kali za mziki mjini Mombasa ambayo imeundwa kwa muundo wa kisasa na inakila kitu kinachohitajika kwa kuzalisha mziki mzuri.

Japo anaonekana mchanga kwenye game la mziki wa kizazi kipya msanii huyo amewaalika wasanii wenye vipaji kutembelea studio yake kukuza vipaji vyao.

 

Show More

Related Articles