BiasharaPilipili FmPilipili FM News

Mbinu Mpya Zakuwavutia Watalii Katika Kaunti Ya Taita Taveta Za Vumbuliwa

Kama njia moja ya kuboresha utalii kaunti ya Taita Taveta wadau wa sekta hiyo sasa wameweka mikakati ya kuvutia watalii kutoka nchini na nje ya nchi.

Meneja mkuu wa  Sarova Taita Hills Game Lodge  Willy Mwadilo anasema kati ya mikakati wanayoweka ni kutambua na kuhifadhi vyombo muhimu vilivyotumiwa zamani wakati wa vita vya kwanza vya dunia.

Anasema pia wametambua maeneo 13 muhimu kwa utalii wa maonyesho ya viwanja vya vita vya kwanza vya dunia eneo hilo.

Mwadilo ameiomba serikali ya kitaifa na ile ya Taita Taveta kuwa na mipango mwafaka ya kulinda na kuhifadhi viwanja hivyo.

 

 

Show More

Related Articles