HabariPilipili Fm

Matokeo Ya KCSE Kutangazwa Leo.

Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa KCSE mwaka uliopita yanatarajiwa kutangazwa hii leo.
Zaidi ya watahiniwa elfu 525 walifanya mtihani huo idadi ambayo ni ongezeko la asilimia 8.3 kutoka wanafunzi elfu 485 waliofanya mtihani huo mwaka 2014.
Waziri wa elimu dkt Fred Matiangi anatarajiwa kuyatangaza matokeo hayo.
Ikumbukwe kuwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka jana walikuwa na muda mfupi wa kujitayarisha baada ya walimu kushiriki mgomo wa kitaifa kwa takriban majuma matano wakishinikiza nyongeza ya mshahara kwa asilimia 50 hadi 60.
Hata hivyo wakati wa mtihani huo visa kadhaa vya udanganyifu viliripotiwa

Show More

Related Articles