BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Masata Wa Bongo Waomboleza Kifo Cha Mzee Majuto.

 

Mchekeshaji Mkongwe kutoka nchi jirani ya Tanzania King Majuto amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akipokea matibabu kwenye Hospitali kitaifa ya Muhimbili nchini humo.

Baadhi ya masta kutoka bongo wameonesha kuguswa na msiba huo kupitia mitandao ya kijamii akiwemo Alikiba aliyechapisha ujumbe huu

“EWE MWENYEZI MUNGU HAKIKA MZEE WETU AMRI BIN ATHUMAN (KING MAJUTO) YUKO KATIKA DHIMA YAKO NA KAMBA YA UJIRANI WAKO, BASI MKINGE NA FITINA YA KABURI NA DHABU YA MOTO NAWE NDIWE MSTAHIKI WA UTEKELEZAJI NA UKWELI MSAMEHE NA UMREHEMU HAKIKA WEWE NI MWINGI WA KUSAMEHE, MWINGI WA KUREHEMU.AMIN”
#SUPPORTEDBYKIBA

Kupitia ukurasa wa Instagram Mwigizaji wema Sepetu pia kachapisha ujumbe wakutia nguvu familia ya marehemu

ALIPANGALO ALLAH… I WISHED TO WORK WITH YOU BABA ANGU… ILA ALLAH HAKUPANGA… KAPUMZIKE BABA ANGU… MUNGU MKALI JAMANI….😔😔😔… ILA KAMA KUTESEKA TU UMETESEKA JAMANI…. RIP KING.”

Muigizaji huyo alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9.

Show More

Related Articles