HabariPilipili FmPilipili FM News

Maktaba Ya Umma Kuimarisha Elimu Taita Taveta.

Viwango vya elimu vinatarajiwa kuimarika mjini VOI na viunga vyake katika kaunti ya Taita-Taveta kutokana na kuzinduliwa kwa maktaba ya umma eneo hilo.

Tayari vitabu elfu 5 vimenunuliwa kwa ajili ya mradi huo unaolenga kufaidisha wanafunzi kutoka familia masikini.

Mbunge wa Eneo hilo Jones Mlolwa anasema iwapo wanafunzi watautumia mradi huo ipasavyo utasaidia pakubwa kuimarisha viwango vya elimu.

Show More

Related Articles