BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Kuna Mtu Ana Nia Ya kuvunja Uhusiano Wangu Na Ali Kiba, Brown Asema.

Msanii wa kizazi kipya kutoka eneo hili la pwani brown mauzo adai  kua kuna mtu aliye na nia ya kuvunja uhusiano wake na star wa bongo Ali Kiba.

Hii ni baada ya kazi waliofanya pamoja kwa jina #Kigoro kuvuja kwa njia isio eleweka na kuanza kuchezwa katika radio mbali mbali katika kanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza na Rais wa umbea Gates Mgenge ndani ya #mwakeMwake brown amelaani vikali kitendo hicho akielezea kutojua jinsi  gani  wimbo huo  ulivyo fikia vyombo vya habari.

“MIMI SIJUI HIYO NGOMA ILIFIKIA MEDIA VIPI SASA SIWEZI ELEZEA IWAPO NI MANAGEMENT  YANGU   YA KITAMBO JIJINI NAIROBI ILIYO ITOA WALA NI STUDIO NILIO REKODI NAYO HUKO DAR. WOTE WAMEKANA  HATA NA SHINDWA KWANI ILIJITOA.”  BROWN KASEMA.

Brown sasa ametoa wito kwa vyombo vya habari kusitisha kucheza kazi hiyo mara moja kwa kile amekitaja kua wakati ufaao wa kazi hiyo kuachiwa haujafika kwani Ilikua katika hatua zake za mwisho mwisho.

“TULITAKA KUIACHIA KAZI HIYO I IKIWA PAMOJA NA VIDEO  SASA ONA MTU ALIAMKA TU NAKUITOA BILA HATA SISI KUJUA MIMI NINGEOMBA RADIO ZOTE ZINAOICHEZA ZIACHE KUICHEZA MARA MOJA. HADI PALE TUTAIACHIA TENA RASMI” . BROWN KATOA WITO.

Wakati uo huo  Brown ameomba msamaha kwa wafuasi  wake  iwapo  hatua hiyo imewakwaza na kuahidi kuachia kazi nyingine  safi  akiwa solo wiki chache zijazo.

Baadhi ya wafuasi wake tuliozungumza nao ameonesha kupendezwa na kazi hiyo. Ambayo wengi wameichukulia kama ujio wake wa pili, baada ya kwenda kimya kwa mda wa takriban mwaka mmoja. Ikumbukwe Kigoro ni kazi ya pili Brown mauzo na alikiba kuwahi fanya pamoja.

 

 

 

Show More

Related Articles