HabariPilipili FmPilipili FM News

Kucheleweshwa Kwa Fedha Za Maendeleo Ndio Chanzo Cha Kudorora Kwa Elimu Nchini.

Kuchelewa kwa  mgao wa hazina ya kitaifa ya ustawishaji wa maeneo bunge NGCDF kutoka kwa serikali kuu umetajwa  kuchangia katika kudidimiza sekta ya elimu nchini.

Hii ni kauli ya mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime akisema kuwa wanafunzi wengi kutoka kwa familia zisizojiweza hutegemea mgao huo kwa basari, pamoja ukarabati na ujenzi wa majengo ya shule.

Mwadime hata hivyo amewalaumu wakaazi kwa kukosa kujitokeza katika mabaraza ili kuchagua kamati mbalimbali za elimu jambo ambalo linachangia wanafunzi wengi kutoka familia maskini kukosa kufaidi mgao huo.

Show More

Related Articles