HabariPilipili FmPilipili FM News

KNEC Imefutilia Mbali Matokeo Ya KCSE Ya Wanafunzi 3,427.

Baraza la mitihani nchini KNEC limethibitisha kufutiliwa mbali matokeo ya mtihani wa KCSE kwa wanafunzi 3,427 katika matokeo ya mwaka jana.

Wanafunzi 1,275 waliponea kufutiliwa mbali matokeo yao baada ya uchunguzi wa kina kuthibitisha hawakuhusika na udanganyifu.

Baraza hilo linasema limelazimika kuchukua uamuzi ili kuweka nidhamu katika wizara ya elimu.

Hata hivyo kama njia ya kuonyesha kujali baraza hilo limesema wanafunzi walioathirika wanaweza kujisajili na kufanya tena mtihani wa KCSE mwaka huu wa mwaka 2019.

Haya yamethibitishwa na George Magoha mwenyekiti wa baraza hilo.

Show More

Related Articles