BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Kelechi Africana Kuzindua Album Mwakani.

Kwa muda mrefu sasa tasnia ya pwani imekua ikipanda na kushuka huku kwa mbali kukionekana na mgawanyiko Fulani hivi wa kimawazo kuhusiana na matamasha na wengine kulalamika kutopewa nafasi yakuwekwa kwenye matamasha tofauti.

Lakini sasa tasnia ya pwani imechukua mkondo tofauti haya nikulingana na meneja wa Kelechi Africana , Athman Babaz ambaye amedokezea meza yetu kuwa kwa sasa wanapanga tamasha kubwa mwakani, tamasha la uzinduzi wa album ya msanii huyo ambaye kiukweli mwaka 2018 umekua wa neema kwake.

Yes 2019 utakua mwaka wa maendeleo zaidi kwani mimi na team yangu twajiandaa kufanya uzinduzi wa album kitu ambacho hakijafanyika Coast na pia si uzinduzi tu bali kuweka historian kwa kufanya kitu cha ajaabu sana. Amesema Athman Babaz .

Kwa mwaka huu msanii huyo ametoa vibao vingi ambavyo kwa asilimia kubwa vimevuma.

Vibao hivyo ni pamoja na Love me, Nimechoka, Wataisoma number ,Digo Love, Wapotezee na sasa anatamba na kibao kipya Nasubiri.

Kulingana na Babaz nikuwa anamalengo yakuhakikisha msanii huyo anavuma anga za afrika mashariki  kwani amaepanga kutoa vibao kwa ushirikiano na wasanii wakubwa kutoka humu nchini na Tanzania.

Kelechi ni mmoja ya wasanii ambao wanaweledi wa uandishi mzuri wa mashairi na pia anaweza kuzalisha nyimbo zake yeye mwenyewe bila kutegemea producer mwengine.

 

Show More

Related Articles