BiasharaPilipili FmPilipili FM News

Gavana Wa Kaunti Ya Taita Awaomba Vijana Kuzingatia Nidhamu Katika Biashara.

Wito umetolewa kwa vijana kaunti ya Taita Taveta kujiunga kwenye vikundi ili wafaidike na mikopo kutoka kwa benki na taasisi za mikopo ya kibiashara.

Wito huu umetolewa na gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja, baada ya kupeana pikipiki 20 kwa chama cha ushirika cha Wumingu-Kishushe riders Sacco.

Samboja amewataka vijana kuzingatia nidhamu katika biashara, na kujiwekea faida na akiba itakayo wasaidia kukidhi mahitaji yao.  Mpango huo unalenga zaidi makundi ya kinamama na vijana kuwawezesha kuendeleza biashara zao mashinani.

Show More

Related Articles