BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Dola Ndio Chanzo Cha Harmonize Kutotumbuiza Eldoret.

Msanii kutoka Tanzania Harmonize kukosa kutumbuiza mjini Eldoret kumeendelea kuzua gumzo mitandaoni huku wengi wakimlaumu aliyeandaa tamasha hilo huku wengine wakilaumu upande wa Harmonize.

Kuleta mwanga kwa kizungumkuti chote sasa event organizer Omondi Wa Mercedes ameweza kujitokeza na kuelezea hali ilivyokua mjini Eldoret.

Mr Omondi amesema kwanza kitambo Harmonize afike Kenya walimlipa dola za kimarekani elfu sita kama hela za mwanzo.

Mambo yalikua sawa mpaka wakati wa sound check na kila mtu alijua swala zima la kutumbuiza lilikua shwari  kwani walikua wamemuongezea  dola nyengine 3,000 alizotaka Harmonize na kufika dola elfu tisa ukijumuisha na zile za mwanzo.

Berfore kufika kwa ukumbi msanii huyo alitaka kukamilishiwa hela zake zilizobaki ila kwa kigezo kimoja tu hela hizo ziwe dola za kimarekani wala si za Kenya.

Mr Omondi aliwarai mpaka wakakubali kuchukua hela za Kenya.

Mimi naeza sema Harmonize alikua ananidai siezi kataa na swala zima nilikua nalisimamia vizuri mpaka pale mmoja wetu kwa jina Jeff alipotuendea kinyume na kusepa na baadhi ya hela ambazo tulitarajia kumlipa Harmonize.

Ila kupitia mahojiano ya simu ndani ya kipindi cha Mwake Mwake meneja wa Harmonize Joel pia ameweka wazi issue nzima huku akisema mwandalizi wa tamasha hilo Mr Omondi hana makosa lakini wendani wake ndio walimtenda lakini hadi sasa yeye hana shida na Omondi.

Jeff aidha amemshukuru Omondi kwa kuwawezesha kurudi Tanzania baada ya kuclear bills zote na pia kuwalipia nauli ya ndege.

Show More

Related Articles