MichezoPilipili FmPilipili FM News

Chapa Dimba Na Safaricom Kuanza Rasmi Wikendi Hii.

Mashindano ya kanda 8 ya chapa dimba na safaricom ambayo ni makala ya pili mwaka huu yataanza rasmi wikendi hii kwenye uga wa Bukhungu kaunti ya Kakamega.

Mshindi wa kipute hicho ataiwakilisha kanda ya Magharibi mwanchi katika mashindano makubwa ya kanda zote nane nchini kaunti ya Meru.

Bingwa mtetezi wa eneo la Magharibi kwa upande wa kinadada Bishop Njenga kutoka Lugari watakipiga dhidi ya Brenda kutoka Bungoma huku Kigandole kutoka Busia watakabiliana na Ibinzo yakutoka Kakamega.

Kwa upande wa wavulana awamu ya nusu fainali Ebbu Stars kutoka Vihiga watavaana na the saints kutoka Butere-Mumias huku Lugari Blue watakipiga dhidi ya Bukembe Friends kutoka Bungoma.

Rais wa shirikisho la soka nchini FKF Nick Mwendwa amesema hatua ya safaricom kuja na mpango huo ni kuhakikisha talanta kutoka mashinani zinavumbuliwa huku akitaja jumla ya wachezaji 15 wanashiriki ligi kuu ya humu nchini pamoja na ile ya NSL baada ya kutambuliwa kutokana na mashindano hayo ya chapa dimba

Mshindi wa jumapili atajishindia shilingi laki mbili na kujiwekea nafasi yakushiriki mashindano ya kila eneo nchini ambayo mshindi wake atajishindia shilingi milioni moja.

Ikumbukwe kuwa wasakaji vipaji kutoka La liga watakua kwenye mashindano hayo kutambua vipaji.

Baada ya Kakamega mashindano hayo yataelekea Kisumu kwa fainali za Nyanza kuanzia tarehe 9 hado 10 mwezi ujao kwenye uga wa Moi Stadium kisumu.

Baada ya hapo itakua ni zamu ya Bonde la ufa ,Mashariki , Pwani , Eneo la kati , Kaskazini Mashariki na Nairobi

 

 

Show More

Related Articles