BiasharaPilipili FmPilipili FM News

Ada Yakulipia Stima Yatarajiwa kupungua kuanzia mwezi ujao.

Tume ya kudhibiti matumizi ya kawi nchini imeondoa ada maalm ya kawi ya shilingi 150 kila mwezi ambayo hutozwa wateja wa KPLC  kila mwezi ikisema sasa wakenya  watalipa ada waliyotumia pekee katika matumizi yao ya kawi wala hakuna ada zaidi watakayolipa kwa shirika la KPLC.

Tume hiyo inasema pia imeondoa ada zengine za kudumu ili kuona wateja wake wanapunguziwa mzigo wa ada pamoja na kuleta usawa katika malipo yao ya huduma ya umeme.

Zoezi la kuondolewa kwa ada hii ya shilingi 150/- almaarufu kama (fixed charge) itaanza rasmi tarehe 1 Agosti .

 

Show More

Related Articles