MakalaPilipili FmPilipili FM News

Mfanyibiashara Aliyetaka Kumhonga Gavana Sonko Kufikishwa Mahakamani Leo.

 

Mfanyibiashara mmoja aliletaka kumhonga Gavana wa Kaunti ya Nairobi Mike Sonko anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya Mombasa hii leo.

Mshukiwa huyo kwa jina Prafull Kumar alitiwa mbaroni hapo jana na maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi Nchini EACC katika  makazi ya gavana Sonko eneo la kanamai kaunti ya kilifi akiwa na shilingi milioni  1 akiwa na nia ya kumhonga gavana  Sonko  ili kupewa idhini ya kuendelea kujenga hoteli yake katika kaunti ya Nairobi.

Kisa hiki kilidhibitishwa na  Afisa mkuu wa tume hiyo pwani kusini George Ojowi.

Show More

Related Articles