Wambani Atuzwa Kama Mchezaji Bora Wa Mwezi Februari.

Wambani Atuzwa Kama Mchezaji Bora Wa Mwezi Februari.
Clavery Khonde

Mchezaji kinda mwenye umri wa miaka 18 wa timu ya Bandari Fc Anthony Wambani amekabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Februari.

Mchezaji huyo ambaye alipachika mabao mawili dhidi ya Sofapaka ametuzwa shilingi laki moja pesa taslimu kwa hisani ya  chama cha muungano wa waandishi wa michezo nchini SJAK pamoja na udhamini wa SportPesa huku pia akituzwa runinga ya nchi 49 kutoka kwa kampuni ya LG.

Also read:   Asilimia 80% ya mamlaka ya bandari ya Mombasa imenyakuliwa

Wambani amewashukuru wachezaji wenzake pamoja na uongozi mzima wa timu ya Bandari kwa kufanikisha ari yake ya mafanikio katika timu hio wawakilishi pekee kanda ya pwani.

Alimfunika Meddie Kagere wa Gor Mahia  ambaye pia aliteuliwa katika tuzo hio.

Wakati huohuo mkufunzi mkuu wa timu  hio Ken Odhiambo amedokeza kuwa ukakamavu na bidii katika mazoezi ndicho kiini cha mafanikio kwa Wambani huku akiwaahidi mashabiki wa kilabu hio mwaka huu utakua wa mafanikio makubwa na wanaimani watashinda taji.

Also read:   Bandari Yateua Afisaa Mpya Wa Habari

Nayo serikali ya kaunti ya Mombasa kupitia idara ya vijana jinsia na michezo imeahidi kushirikiano vyema na timu hio ili kuhakikisha inapata mafanikio zaidi katika ligi kuu ya KPL msimu huu.

Post source : Clavery Khonde

Related posts

MNL App
MNL App