HabariPilipili FmPilipili FM News

Marwa Anguruma Mombasa.

Katibu katika wizara ya ugatuzi Nelson Marwa amewaonya magavana dhidi ya kujihusisha na ufisadi akisema amejitolea kukomesha ufisadi katika kaunti zote nchini.

Akihutubia washikadau katika kongamano la kupambana na mizozo hapa Mombasa, Marwa amewataka magavana hao kuhakikisha wakenya wanapata huduma sawasawa.

Amewataka magavana hao kuhakikisha wakenya wanahusishwa katika masuala ya maedeleo ya kaunti akisema wizara ya ugatuzi inatafuta njia mbadala ya kutatua mizozo ya kaunti bila ya kuenda mahakamani.

Also read:   The President declare total war on drug abuse at the coast

 

Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker