Marwa Aombwa Kumtimua Naibu Kamishna Eneobunge la Jomvu.

Marwa Aombwa Kumtimua Naibu Kamishna Eneobunge la Jomvu.
pilipili photography

Story Highlights

  • Mbunge wa Jomvu Badi Twalib amemtaka aliyekuwa mshirikishi wa serikali kuu Pwani Nelson Marwa kuingilia kati na kuhakikisha kuwa kaimu naibu kamishna eneobunge la Jomvu Elizabeth Ngava, anachunguzwa kwa kile kinadaiwa kuhusika na unyakuzi wa ardhi eneo hilo.

Hii ni baada ya baadhi ya maafisa wa Polisi wa eneo hilo kupatikana wakisimamia shughuli ya kulima barabara katika kipande cha ardhi, kinachodaiwa kunyakuliwa na bwenyenye mmoja eneo la Miroroni Gotani, Suala ambalo Badi anasema linaibua masuali mengi.

Siku chache zilizopita  kiongozi huyo aliwapatia siku 7 mabwenyenye 3 wanaohusishwa na unyakuzi wa ardhi eneo hilo, kuwasilisha hatimiliki ya ardhi zao kwa wizara ya Ardhi kaunti ya Mombasa, la sivyo wakabiliwe kisheria.

Also read:   Mv Jambo Hatimaye Yawasili Bandarini Mombasa.

Post source : pilipili fm news

Related posts

MNL App
MNL App