KFCB Yakamata Matatu 78 Mombasa.

KFCB Yakamata Matatu 78 Mombasa.
Pilipili photography

 

Zaidi ya magari 78 ya umma yanayohudumu ndani ya kaunti ya Mombasa pamoja na madereva na makondakta wao  yametiwa mbaroni na bodi ya kudhibiti filamu nchini KFCB ikishirikiana na maafisa wa polisi kwa kupatikana na kosa la kucheza na kuonyesha filamu za ngono.

Akidhibitisha hili afisa mtendaji wa bodi hiyo eneo la Pwani Bonventure Kioko amesema magari hayo yameshikwa baada ya kupatikana yamekiuka sheria.

Also read:   Main suspect behind the Bella Vista terror attack sentenced to death

Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo nchini Ezekiel Mutua ametoa wito kwa wamiliki magari ya umma kuchukua leseni zitakazotoa muongozo wa yale yanayofaa kusikilizwa na kuonyeshwa kwenye magari hayo.

 

Post source : Pilipili fm news

Related posts

MNL App
MNL App