Msanii Radio Kutoka Uganda Afariki.

Msanii Radio Kutoka Uganda Afariki.
pilipili photography

Msanii mkubwa kutoka Uganda Moses Ssekibongo almaarufu kama Mowzey  Radio amefariki dunia asubuhi ya leo akipokea matibabu katika hospitali kuu jijini Kampala.

Kifo cha nguli huyo wa mziki nchini humo kimethibitishwa na mmoja wa mameneja wake Balaam Barugahare ambaye amesema ni kweli Radio alipumua hewa yake ya mwisho mida ya saa mbili na robo asubuhi.
“Yes Radio is gone he died at 6:00am this morning “Amesema meneja huyo.

Also read:   Atongoria ngurani a kimabururi kwendithiria President Uhuru utongoria mwega

Radio alilazwa katika hospitali ya Kampala baada ya kupata majeraha mabaya kutokana na kile kilichotajwa kupigwa katika sehemu moja ya burudani nchini humo.

Taarifa za vyombo vya habari nchini Uganda zinasema Radio alipigwa hadi kupoteza fahamu na alikua mahututi wakati akipelekwa hospitalin.

Kifo cha msanii huyo kinajiri masaa machache tu baada ya rais Yoweri Museven kutoa milioni 30 za Uganda ambazo nisawia na 856,000 pesa za Kenya.

Also read:   Msemaji wa polisi Uganda Feliz Kaweesi auwawa

Wiki iliyopita polisi nchini humo walisema waliwakamata watu watanano wanaodaiwa kuhusika na kisa hicho.

Mowzey Radio alikua member wa kundi la Radio and Weasel kundi ambalo lilitoa vibao vikali kama vile Bread and butter,Zuena,Magnetic na Don’t cry waliomshirikisha Wizkid kutoka Nigeria.

Sisi kama meza ya Soga za usanii tunasema Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi Amin.

Post source : pilipili fm news

Related posts

MNL App
MNL App