Mbunge Wa Mvita Atoa Wito Kwa Wazazi Kupeleka Watoto Shuleni

Mbunge Wa Mvita  Atoa Wito Kwa Wazazi Kupeleka Watoto Shuleni
pilipili photography

Mbunge wa mvita Abdulswamad Sharrif  Nassir ametoa wito kwa wazazi wote eneo la mvita kuhakikisha watoto wao wamejiunga na shule za upili, ikizingatiwa kuwa serikali imetenga fedha za ziada kwa wanafunzi.

Ameongeza kuwa  wiki ijayo wataandaa mikutano na walimu wakuu wa shule za upili za kaunti ya mombasa kuhakikisha wazazi waliolipa karo wamerejeshewa pesa zao.

Also read:   Kamati Kubuniwa Kushughulikia Ruwaza Ya 2035 Mombasa.

Hata hivyo wazazi wameiomba serikali ya kaunti ya mombasa kuangalia   shule ambazo zimejengwa katika mazingira mabaya, hasa yenye makundi ya uhalifu  wakisema hali hiyo inahatarisha maisha ya wanafunzi wengi , na hata kuathiri masomo yao.

Haya yanajiri wakati kaunti za pwani zikiandikisha idadi ndogo ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza, huku kaunti za kilifi na kwale zikiongoza kwa hali hiyo.

Also read:   Mahakama ya kisasa kujengwa kaunti ya Mombasa

Post source : pilipili fm

Related posts

MNL App
MNL App