Wema Sepetu Ni Meneja Wangu Mpya, Asema Dogo Richy

Wema Sepetu Ni Meneja Wangu Mpya, Asema Dogo Richy
pilipili photography

Baada ya kutoa mziki majanga na kurudi kwenye upeo wa tasnia ya mziki nchini Kenya msanii Dogo Rich sasa amerudi tena na jipya na round hii ni kuhusu usimamizi wa mziki wake.

Katika mahojiano kwenye kipindi cha Mwake Mwake Live na Gates Mgenge msanii huyo ameweka wazi kuwa kazi zake zitakua zikisimamiwa na mwanamitindo na muigizaji maarufu afrika mashariki mwanadada Wema Sepetu.

Haya yanajiri baada ya video kuvuja kwenye mtandao wa mwanamitindo huyo akiimba na kucheza ngoma mpya ya Dogo Richy iitwayo Follow Me.

Akiulizwa msanii huyo ameweka wazi kuwa sasa mambo yako sawa na nikutoa kazi baada ya nyengine.

Kwa sasa Dogo Richy anasimamiwa na king kong entertainment  lakini ameweka wazi kuwa Wema atahusika katika usimamizi na usambazaji wa mziki wake.

Post source : pilipili fm news

Related posts

MNL App
MNL App