BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Majini Yamlazimisha Susumila Kuyaimbia.

Katika siku za nyuma msanii kigogo kutoka Mombasa Yusuf Kombo almaarufu Susumila kwa jina la usanii amehusishwa na ushirikina huku mke wake wa kwanza kuna time aliweka wazi kuwa msanii huyo anaabudu nguvu za giza na hushiriki ushirikina sana katika kazi zake za kisanii.

Wengi walipuuzia wakamuona muongo na hata kumuona pia msaliti, kuna wakati pia msanii mwenzake Chikuzee ambaye walishafanya kazi wote katika studio za Honet wakati huo chini ya produza TK2 nakutoa vibao vikali Hidaya Na ngoma itambe pia alitoa lalama kama hizo akisema Susumila ni mchawi na huchukua nyota za wenzake katika kazi za usanii.

Also read:   Consistence Ndio Dawa Ya Mziki,Asema Susumila.

Wengi pia wakapuuzia wakamuona Chikuzee ameishiwa na makali hivyo alikua anatafuta kiki.

Lakini sasa imedhihirika wazi kuwa msanii huyu mkali anaamini nguvu za giza na hata kuabudu ushirikina, hili limebainika katika utunzi wake wa hivi punde ambapo katika nyimbo yake mpya ambayo anatarajiwa kuidondosha wiki mbili zijazo masanii Susumila amesifia sana ushirikina huku akitaja maneno ambayo hutumiwa na watu ambao huamini nguvu za giza.

Also read:   Susumila Ahidi More Music Kwa Mafans Wake

Katika ngoma hio mpya ambayo meza yetu ya soga ilifanikiwa kuiskiza pia inamnukuu Susumila akishukuru jinni aina ya subihan akisema limemsaidia kupata gari, umaarufu kimziki, wanawake wazuri wakati huo huo akisema pete pia amelivalisha na kulipaka marashi ya pemba ili litulie.

Nyimbo hio mpya ambayo msanii huyo anatarajia kuitoa inakwenda kwa jina Tawire.

 

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker