Wasanii Wawili Watemwa Toka Wasojali Band

Wasanii Wawili Watemwa Toka Wasojali Band
Pilipili photography

Wanasema heshima ndio msingi wa kila kitu katika maisha hususani kazini lakini swala hilo kwa baadhi ya wasanii limekua kinyume kwani wamekua wakionyesha kibri na hata kuwasahau wanaowasaidia kimziki.

Kama wewe ni mdau wa tasnia ya mziki kanda ya pwani basi bila shaka nikikutajia kundi la Wasojali Band moja kwa moja utakumbuka nyimbo kama vile Nitalia Nawe, Aumbora, Jirani na wacha waseme na bila shaka ulidhani kundi hili lingefata nyendo za yamoto band toka kule Tanzania lakini hali nitofauti kufikia sasa.

Also read:   Rais awaonya wanasiasa dhidi ya kuwashawishi wakenya

Mkurugenzi mkuu wa Kubwa Entertainment  Athman Babaz amejitokeza wazi nakusema baadhi ya wanachama wa kundi hilo ambao ni E-Driss wasojali na Hamso wasojali hawako tena katika kundi hilo kwa sasa.

“Wasanii hao wawili walionyesha dharau licha ya kuwasaidia na hata kuwakodishia nyumba but at the end wakaamua kusepa bila hata kunambia so ndo hivyo sasa hivi najaribu kuunda tena kundi hilo”. Amesema Athman Babaz.

Mkurugenzi huyo ameonyesha masikitiko yake lakini hata hivyo akaapa kutokufa moyo katika azima yake ya kusimamia wasanii.

Also read:   Arwaru 6 gukua thibitari-ini nene ya Gicua-ini kurumirira mugomo wa arigitani

Kwa sasa Athman Babaz amejitosa katika uproducer na amejibandika jina la producer Lechi na ngoma ya kwanza ambayo ameifanya yeye kama producer ni Sina ya Kelechi Africana.

 

Post source : Pilipili fm news

Related posts

MNL App
MNL App