Schweinsteiger Aihama Manchester United.

Schweinsteiger Aihama Manchester United.
Photo: pilipili photography

Mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Ujerumani ambaye ni mshindi wa kombe la dunia la mwaka 2014 Bastian Schweinsteiger amekatisha ndoa yake na kilabu ya uingereza ya Manchester United na kutia saini na kilabu ya marekani Chicago Fires inayoshiriki ligi ya MLS.

Kilabu hio ya marekani ilithibitisha Jumatatu kuwa nguli huyo mwenye umri wa miaka 32 ni kweli amesaini mkataba na Chicago na anatarajiwa kuungana na kikosi cha Veljko Paunovic wiki ijayo.

Mchezaji huyo ambaye alikua amekosa nafasi ya kudumu kwenye jeshi la Manchester United linaloongozwa na Jose Mourinho sasa atatia kibindoni dola milioni 4.5 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2017 kwenye kilabu yake hio mpya.

Also read:   Man United Ndio Mabingwa Wa EFL CUP.

Katika kazi yangu ya uchezaji hua Napata nafasi ambazo hua ninaimani nitaleta mabadiliko amesema kingo huyo kwenye taarifa maalum huku akisema kilabu hio ya Chicago inamalengo mazuri na baada ya kuongea na mkurugenzi wa Chicago Nelson Rodriguez nimepata imani na soka langu tena ameongezea Schweinsteiger

Schweinsteiger hajatumiwa sana msimu huu katika kilabu ya Manchester United na amecheza mechi 11 pekee msimu huu kwenye mashindano yote.

Also read:   Rais Kenyatta Ataka Wizara Za Kilimo Na Usafiri Kuelezea Uhaba Wa Unga Wa Mahindi.

Kabla ya kujiunga na kilabu ya united mchezaji huyu alikuwa ametumikia miamba ya soka ya ujerumani Bayern Muchen tangu mwaka 2002, na alitundika daluga msimu uliopita na kuacha kuichezea timu ya taifa ya ujerumani mara tu baada ya mtinange wa kifiki dhidi ya Finland Agosto 31 mwaka jana.

Ameifungia ujerumani mabao 24 kwenye mechi 121 alizoshiriki ikijumuishwa mechi sita za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil ambako walibeba kombe hilo.

.

 

Post source : pilipili fm news

Related stories