Wakaazi Wa Kwale Watkiwa Kuzingatia Umoja.

Wakaazi Wa Kwale Watkiwa Kuzingatia Umoja.
Photo: pilipili photography

Wakazi wa Kaunti ya Kwale wamehimizwa kuzingatia umoja na wakatae kugawanywa kwa misingi ya ukabila na baadhi ya viongozi wanaoeneza siasa za chuki.

Akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mkongani alipoongoza ufunguzi rasmi wa jengo la nyumba za madaktari wanaohudumu eneo hilo, Gavana wa Kwale Salim Mvurya ametoa tahadhari kwa wananchi akisema wapo baadhi ya wanasiasa wanaoeneza propaganda, kuhusu suala la ajira katika Kaunti hiyo.

Also read:   Maradhi ya Kalazaar : Bado kuna changamoto na uhaba wa fedha katika kukabiliano nao

Kuhusu suala la uboreshaji huduma za afya katika eneo hilo, Gavana Mvurya amedokeza kuwa karibuni Serikali ya Kaunti itaanzisha mradi wa ujenzi wa jengo la kisasa la kuwahudumia wagonjwa ili hospitali hiyo ipandishwe daraja.

 

Post source : pilipili fmnews

Related stories