People Daily

Ayacko aeleza hofu kuhusu visa vya hitilafu za kimitambo katika vituo vya upigaji kura

Mgombea kiti cha useneta kaunti ya Migori Ochilo Ayacko ameelezea hofu kuhusu visa vya hitilafu za kimitambo katika vituo kadhaa vya upigaji kura kaunti hiyo. Ayacko ameitaka tume ya IEBC kuangazia tatizo hilo kwa dharura ili kufanikisha zoezi hilo. Hata hivyo ameelezea kuridhishwa na hali ya usalama. Naye mwakilishi kina Mama Florence Mutua ameelezea imani ya kuwa ODM itaibuka mshindi katika uchaguzi huo huku pia akiwahimiza wapiga kura kujitokeza kwa wingi.

Show More

Related Articles