BurudaniPeople DailyPilipili FmPilipili FM News

Msanii Wa WCB Alichukua Mashairi Yangu Kutunga Nyimbo Yake, Asema Dogo Richie.

Ni jambo la kawaida kwa wasanii mashairi yao kwa kiasi fulani kuoana na hili hutokea pia kwa wazalishaji wa mziki (Producers) kupiga key ambazo sometimes hufanana.

Msanii kutoka Mombasa Dogo Richie mkali wa ngoma za Fire na Go gaga ametoa kilio chake siku chache tu baada ya msanii wa WCB Lava Lava kuachia ngoma yake mpya ya Go gaga ambayo si kufanana tu kwa jina bali kwenye nyimbo hio kuna baadhi ya stanza ambazo Dogo Richie aliziimba katika ngoma yake ya Fire na Go gaga na Richie ametoa kauli yake akisema yes mashairi hufanana lakini hili la Lava lava kutumia baadhi ya mashairi ya nyimbo zangu mbili kuunda ngoma yake sielewi kabisa.

 

Ngoma nimeiskiza ni nzuri na kitu ambacho msanii huyo wa WCB amenishindia maybe nitasema ni kichupa kizuri cha video na nakshi nakshi but kwa mashairi tupo sawa, Amesema Richie.

Nyimbo ya Go gaga ya Dogo Richie iliachiliwa mwezi uliopita na yaendelea kufanya vizuri huku msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo mpya ya Milele amedokeza  ataendelea kukaza kuhakikisha mziki wake unafika mbali.
Alipoulizwa kuhusu ujio wa Lava Lava, Richie amesema ngoma ni nzuri na anashukuru kwa ujio huu utamunufaisha kwa sababu watu wameanza kumutafuta na kutaka kujua kuhusu kazi zake.

Ok ni kweli nimepata jumbe nyingi sana pia kuna wasanii wakubwa tayari wameanza kuniulizia baada ya taarifa kusambaa kuwa ngoma ya Lava Lava kutoka ikionekana kufanana na yangu. Ameongezea msanii huyo.

.

Dogo Richie ameongezea kuwa hana maana  Lava Lava  hawezi kutunga lakini hii yake ni kali sana yakuchukua line za nyimbo mbili tofauti na  kuunda yake yuko sawa sana na namvulia kofia kwa ubunifu wake huo.

Show More

Related Articles