People Daily

Mswada Wa Kuvunjiliwa Mbali Kwa Kampuni Ya Usambazaji Maji Ya Kwale Wapitishwa.

Bunge la kaunti ya kwale limepitisha ripoti ya kutaka  kuvunjiliwa mbali kwa kampuni ya huduma za usambazaji  maji ya kwale KWAWASCO kwa madai ya kushindwa kujisimamia.

Ripoti hiyo iliwasilishwa na mwenyekiti wa kamati ya matumizi ya fedha za umma  katika bunge hilo Patrick Mangale,  na ilipendekeza kuvunjwa kwa kampuni hiyo kutokana na madai  kuwa  usimamizi  wa kampuni hio umesheheni ufisadi   hatua  inayopelekea kushindwa  hata kulipa mishahara ya wafanyikazi wake.

Also read:   Mkurugenzi Wa Maji Kwale Atuhumiwa Kwa Utepetevu Kazini.

Wajumbe hao wamependekeza majukumu ya kampuni hiyo kuchukuliwa na serikali ya kaunti chini ya wizara ya maji huku wafanyikazi wake wachujwe na kuajiriwa na serikali hiyo.

Haya yakuja huku kampuni hiyo ikisemekana kudaiwa zaidi ya milioni 100 na bodi ya maji pwani na zingine milioni 36 na mamalaka ya ukusanyaji ushuru humu nchini.

Also read:   Wananchi Walalamikia Uhaba Wa Maji Malindi.
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker