K24 TvNEWSSwahiliVideos

MASHUJAA WA UHIFADHI WA MAZINGIRA WAKUMBUKWA

Waziri wa Utalii na Wanyama Pori, Najib Balala, amelitaka Shirika la Wanyama Pori KWS, kuwaajiri watu kutoka familia za walinzi wa wanyama pori waliopoteza maisha yao katika vita dhidi ya uwindaji haramu au kuuawa na wanyama hao.

Akizungumza Jumapili, katika hafla ya kuwaenzi mashujaa wa ulinzi katika mbuga ya wanyama pori nchini, mama wa taifa Bi. Margaret Kenyatta amewapa kongole walinzi wote wanaojitolea kuhakikisha wanyama pori na binadamu wanatangamana ipasavyo na pia kuendeleza vita dhidi ya ujangili.

Show More

Related Articles