HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya watu 35 wakesha nje baada ya nyumba zao kuteketea mjini Maua

Zaidi ya watu 35 wamelazimika kukesha  kwenye kijibaridi katika mji wa Maua baada ya moto kuteketeza makaazi yao usiku wa kuamkia leo.

Kulingana na walioshudua mkasa huo, moto wenyewe ulianza mwendo wa saa saba usiku na juhudi za kuukabili  zilikosa kufua dafu.

Wanaisuta serikali ya kaunti hiyo kwa kukosa kushughulikia moto huo kwa haraka kufuatia madai kuwa mashine wanayotumia imeharibika.

Chanzo cha moto huo kinasalia kitendawili

Show More

Related Articles