HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya familia 500 zatoroka makwao kutokana na utovu wa usalama Kerio Valley

Zaidi ya familia 500 zimetoroka makwao eneo la Kerio Valley pamoja na maeneo mengine yanayoshuhudia utovu wa usalama kanda ya Kaskazini mwa bonde la Ufa. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kapyegon ,Kamulogon,Tapach,Embobut na eneo la Kerio Valley ambako shule  kadhaa zimefungwa kutokana na ukosefu wa usalama mpakani. Gavana wa Pokot Magharibi John Lonyangapuo wamelaani vikalio mashambuli  hayo na kuitaka idara ya usalama kuimarisha doria na kuwanasa wahalifu wanaohusika. Naye gavana wa Elgeyo Marakwet Alex Tolgos  amewarai wakazi waliohama kurejea makwao akitoa changamoto kwa polisi kuwahakikishia usalama wao.

Show More

Related Articles