HabariMilele FmSwahili

”Wizara ya elimu haiko tayari kuzindua mtaala wa 3.6.6.3 mwaka ujao wa 2019”

Wizara ya elimu  inasema haiko tayari kuzindua mtaala mpya wa 3.6.6.3 mwaka ujao wa 2019. Waziri wa elimu balozi Amina Mohammed anasema  wanaendelea kufanya mashauriano  na wadau tofauti kuhusu mpango huo kabla ya kuanzishwa. Anasema watakaoendesha mpango huo pia wangali wanaendelea  kupewa mafunzo na  ununuzi wa vifaa vitakavyotumika. Mtaala huo unatarajiwa  kuchukua nafasi ya  ule unaotumika kwa sasa wa 8.4.4.

Show More

Related Articles