HabariMilele FmSwahili

Wenyeji wa Baringo kusini waelekea debeni kumchagua mbunge mpya

Wenyeji wa Baringo kusini wanaelekea debeni asubuhi hii kumchagua mbunge mpya atakayemrithi Grace Kipchoim aliyefariki akipokea matibabu katika hospitali moja hapa jijini Nairobi mwezi aprili. Tayari vituo vya kupiga kura vimeanza kufunguliwa maeneo 132 eneo bunge hilo likiwa na wapiga kura 35,162 waliosajiliwa. Kinyanganyiro kikali kinatarajiwa baina ya Dkt Cynthia Kipchilat wa Maendeleo Chap Chap na Charles Kamuren wa Jubilee.Mkuu wa IEBC kaunti ya Baringo Hussein Gurre na afisa mkuu wa tume ya uchaguzi Abdi Guliye wametoa hakikisho kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki.IEBC pia inaandaa chaguzi ndogo za wadi za Bobasi Chache na North Kadem

Show More

Related Articles