HabariMilele FmSwahili

Waziri wa barabara kaunti ya Nakuru Lucy Kariuki atimuliwa ofisini

Waziri wa barabara kaunti ya Nakuru Lucy Kariuki ametimuliwa afisini. Ni baada ya wajumbe wa bunge la kaunti hiyo kupasisha hoja ya kutokuwa na imani naye kufuatia madai ya matumizi mabaya ya afisi. Katika kura hiyo iliyopigwa leo, wajumbe 49 wameunga mkono hoja hiyo,21 wakiipinga huku mmoja akisusia. Kutimuliwa kwake kunajiri saa chache baada ya gavana wa kaunti hiyo Lee Kinyajui kufanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri na kumhamishia waziri huyo katika wizara ya maswala ya vijana.hawa hapa wawakilishi wadi baada ya shughuli hiyo.

Show More

Related Articles