HabariMilele FmSwahili

Waziri Magoha awaonya wanaopinga utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu

Waziri wa elimu prof George Magoha amewaonya wanaopinga utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu akisema wanapoteza muda wao. Akizungumza jijini Nairobi wakati alipokuwa akizindua rasmi mafunzo kwa takriban walimu elfu 91 kote nchini, prof Magoha ametoa hakikisho kwamba mtaala huo utafikia darasa la nne kufikia mwezi Septemba mwaka huu.

Aidha Magoha amesema kama wizara watahakikisha mtaala huo unafikia kiwango cha juu kufikia mwishoni mwa mwaka huu na kwamba unalenga kuwanufaisha watoto wote wa jamhuri yakenya bila.

Akizungumza katika hafla hiyo pia, afisa mkuu mtendaji wa tume ya kuwajiri walimu nchini, TSC Nancy Macharia amewahimiza wote wa darasa 1,2,3 na 4 wanaopokea mafunzo hayo kutolipa chochote kupata mafunzo hayo kwani ni ya bure. Amewataka kupuuza walaghai wanaowaitisha pesa.

Mafunzo hayo yanaendelea katika maeneo elfu 1,191  ambapo inaarifiwa walimu wote waliohitajika kupokea mafunzo wamefika. Serikali inalenga kuwapa mafunzo jumla ya walimu elfu 228, 300 wa shule za msingi kufikia mwishoni mwa mwaka huu

Show More

Related Articles