HabariMilele FmSwahili

Waziri Balozi Amina atoa wito kwa wahadhiri wanaogoma kurejea kazini

Waziri wa elimu Balozi Amina Mohamed ametoa wito kwa wahadhiri wanaogoma kurejea kazini. Akizungumza katika chuo kikuu cha Meru balozi Amina amewahakikishia wahadhiri hao kuwa serikali iko tayari kufanya mashauriano na viongozi wao pamoja na wadau mbali mbali kutafuta suluhu. Pia amesema wizara yake inafanya mashauriano na tume ya kuwaajiri walimu kuhakikisha walimu waliotoka Wajir kutokana na sababu za usalama wanarejeshwa
Balozi Amina pia ametoa hakikisho haki itatendeka kufuatia mauaji ya kiongozi wa wanafunzi chuoni humo Evans Njoroge tayari naibu chansella wa chuo hicho cha Meru prof Japheth Magambo ametumwa likizo ya hiari huku nafasi yake ikitwaliwa kikaimu na, prof Charity Gichuki

Show More

Related Articles