HabariMilele FmSwahili

Watu 5 wafariki katika ajali ya barabarani eneo la Longisa barabara ya Narok- Bomet

Watu watano wamepoteza maisha yao huku wengine kumi na wanne wakijeruhiwa katika ajali ya barabarani katika eneo la Longisa barabara ya Narok Bomet.

Inadaiwa kuwa mtu mmoja amefariki katika eneo la tukio huku wengine wanne wakifariki wakipokea matibabu katika hospitali ya Longisa.

Ajali hiyo imetokea pale matatu ya abiria kumi na wanne ya Sacco ya Egesa ilipopoteza mwelekeo. Uchunguzi zaidi unaendelea.

Show More

Related Articles