HabariMilele FmSwahili

Watu 4 wafariki Kieni Nyeri baada ya kula chakula kinachoshukiwa kuwa kibaya

Watu wanne wamefariki huko Kieni Nyeri baada ya kula chakula kinachoshukiwa kuwa kibaya katika sherehe za kulipa mahari.

Wahusika walianza kulalamikia maumivu ya tumbo na kuendesha.Miongoni mwa waliofariki ni mamake kijana aliyekuwa akilipa mahari.

Waathiriwa wengine 100 wanatibiwa katika hospitali  ya Karemeno saba kati yao wakiwa hali mbaya.

Kijana aliyekuwa akilipa mahari naye anatibiwa katika hospitali kuu ya Kenyatta.

Show More

Related Articles